Nikki Atoa Sababu ya Kumchagua na Kumvisha Pete Mpenzi Wake
Mwanamuziki Nikki wa pili ambae wikiendi iliyopita aliamua kuvunja ukimya na kumvisha pete mwanamke aliyekuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu na hata kuanza harakati za kufunga ndoa.
Akiongea na EATV, Nikki anatoa sababu kubwa za kumfanya kuamua kumuamini mpenzi wake huyo na kuamua kumvisha pete huku sababu kubwa akisema kuwa ni mwanamke mwenye mapenzi ya kweli na anaamini kuwa anampenda.
kwanza ananipenda, icho cha kwanzalakini cha pili tunaweza kuelewana tukiwa katika huzuni, furaha na hata maumivu pia.yeye anaweza kuelewa kuwa hapa nikki yuko hivi kwa sababu ya hivi lakini pia anauwezo wa kuelewa kuwa Nikki ana mabaya yake mengi na mazuri pia, kitu ninachiweza kupungukiwa anaweza kujaza.