Harmonize Afungukia Ujauzito Wa Sarah

Msabii wa muziki wa Bongo fleva Kutoka katika Label ya WCB, Harmonize amefunguka na kutoa majibu kuhusu utata wa ujauzito wa Mpenzi Wake Sarah.

Wiki chache zilizopita Sarah alitupia picha zilizomuonesha ni wa kujifungua muda wowote. Kabla ya kutupia picha hiyo kulikuwa na madai na minong’ono mingi kuwa mchumba huyo wa Harmonize alikuwa haonekani mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa huko nyuma kwa sababu eti alikuwa analea mimba hiyo hivyo hakutaka kujitokeza hadharani.

download latest music    

Lakini alipohudhuria Birthday party ya Msanii Wolper Wiki iliyopita na kuonekana akiwa hana ujauzito maneno Mengi yalizuka na kushangaza wengi walioamini mzungu huyo ni mjamzito.

Baada ya kuzidi kwa minong’ono Gazeti la Ijumaa, lilimfuata Mpenzi Wake Harmonize ili kupata ukweli wa mambo ambapo alifunguka:

Sidhani kama kila kitu ni vizuri kukiweka kwenye hadhara. Ni jambo kubwa hilo, lakini ni la kifamilia zaidi.

Kama anavyoonekana, hajajifungua na hana mimba kweli. Mara kadhaa Sarah amekuwa akidaiwa kuwa mjamzito, lakini hazina ukweli”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.