Nikki Wa Pili Amvisha Pete Ya Uchumba Mpenzi Wake
Msanii wa muziki wa hip hop nchini kutoka katika kundi la Weusi Nikki wa pili amemvalisha pete ya uchumba Mpenzi Wake wa siku nyingi anayejulikana kwa jina la Joan.
Bongo 5 wanaripoti kuwa Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi mkoani Arusha nyumbani kwa msanii huyo ambapo rasmi aliaga ukapera.
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na wasanii wenzake Kama vile Kama yake Joh Makini, Dogo Janja, Lord Eyes na Juma Jux.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki wa pili alimuweka Mpenzi Wake huyo na kumsindikiza kwa maneno matamu na kuandika:
Queen, malkia, mwenye moyo wangu…….nuru ya uzuri wako imulike njia ya maisha yetu…..Nakupendaaaa sanaaaaaaaaa #sikuyetu ahadi ya kwanza nimetimiza”.