Pappii Kocha Afungukia Tetesi Za Kubambikiwa Mtoto
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Johnson Nguza Viking maarufu kama Pappii Kocha amefungukia tetesi ambazo zimekuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii ambapo mashabiki zake wamehoji endapo yule ni Mtoto Wake.
Oktoba 28 mwaka huu Pappii Kocha alimuweka hadharani Mtoto Wake ambaye alimzaa mara tu Baada ya kutoka gerezani kwa msamaha wa raisi mapema mwaka huu.
Wapo waliojifanya wanajua kukokotoa mahesabu kwa kumhesabia siku alizotoka jela na kulinganisha na muda wa kubeba mimba kisha kujipa majibu kuwa mtoto huyo si wake kwamba huenda amebambikiwa, lakini wapo waliompongeza na kutaka kumjua mwanamke aliyezaa naye.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Papii Kocha alikana tetesi hizo na kusema kuwa Mtoto Yule ni wa kwake na ana uhakika huo:
Unajua nini? Mimi nilitoka jela Desemba 9, mwaka jana ambapo Desemba 9, mwaka huu (kesho) nitakuwa natimiza mwaka mmoja, na siku niliyotoka nilipokelewa na mama mtoto nikabahatika siku hiyohiyo kumpa ujauzito hivyo naamini mtoto wangu ni wa halali kabisa na niwatoe wasiwasi”.
Papii Kocha tayari ana Mtoto wa kike ambaye ana umri wa miaka 18 aliyemzaa kabla ya kwenda jela Lakini hivi sasa Papii Kocha amekataa kumuweka wazi mwanamke aliyezaa naye.