Juma Nature Amtamani Sana Rayanny
Msanii mkongwe na wa siku nyingi katika game Juma nature , ameshindwa kuficha hisia zake baada ya kuamua kusemwazi kabisa juu ya ufanyajikazi wa msanii rayvanny ambae amekuwa akijituma sana kufanya kazi akitkea katika kundi la wcb.
Juma nature anasema kuwa kama itatokea akapata bahati ya kuchagua ni mtu gani kwa sasa anatakiwa kufanya nae ngoma basi msani wa kwanza kumchagua atakuwa ni Rayvanny kutoka katika kundi la WCB.
Sasa hivi naona vijana wengi wanafanya kazi sana, ila kwa upande wangu mimi , nikipata nafasi nikiwa kama msanii mkubwa nitataka kufanya kazi Rayvanny na kwa sababu ana kipjai sana.
Pia Juma nature anasema kuwa kati ya muziki wa zamani na wa sasa hivi, muziki wa sasa hivi umekuwa na maendeleo makubwa sana kulinganisja na ule wa zamani hata maisha ya wasanii yaebadilika san.