Sheikh Mkuu Amjia Juu Uwoya Baada Ya Kutangaza Msimamo Wake Wa Kidini
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Alhad Mussa amemjia juu Msanii wa Bongo movie Irene Uwoya baada ya kutangaza kwamba hakuolewa kwa dini ya Kiislamu na aliyekuwa mume wake, Dogo Janja.
Sakata hilo lilianza wiki iliyopita Baada ya Uwoya kutoa kauli iliyodai kuwa yeye sio muislam na wala hajawahi kubadilisha dini alipofunga ndoa ya kiislamu na Dogo Janja kama watu wengi walivyodhania.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani Shekhe huyo alisema, kauli ya Uwoya kudai kuwa yeye si Muislamu inaonesha kuwa wakati akibadili hakuifuata dini bali mwanaume.
Mwanadada huyo kuchukua uamuzi wa kutaka kuolewa na aliyekuwa mwenza wake hakuridhia kutoka moyoni, hivyo katika ndoa hiyo Uwoya alimfuata mwanaume na wala hakufuata dini“.
Irene Uwoya alifunga ndoa ya Kiislamu na Dogo Janja na kutangaza kuwa, amebadili dini na kuitwa Sheila, hata hivyo baada ya miezi kadhaa wawili hao waliachana kimyakimya bila kuweka wazi ndoa yao kuvunjika.