Tumbo Kubwa La Thea Lazua Utata
Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea alizua gumzo mbele ya hadhara Baada ya kuonekana kuwa na tumbo kubwa kupitiliza.
Kutokana na kitambi hicho mara moja kuna taarifa zilisambaa kwamba huenda mwanamama huyo ni mjamzito na watu wengi ndiyo maana tumbo limemtoka hivyo au kama ni kuridhika na maisha basi ameridhika kwelikweli.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers na kuulizwa kuhusiana na madai kwamba ni mjamzito au laa, Thea alikuwa na haya ya kusema:
Jamani sina ujauzito, hili tumbo ni kwamba nimenenepa tu, yaani nimeridhika na maisha ninayoishi lakini kama watu Wananichuria haina shida kwa sababu kuzaa ni jambo jema sana.”
Mashabiki wengi walionekana kuuponda muonekano wa Thea na kumkosoa kwa kujiachia na kunenepeana tu na kupoteza mvuto Wake Kama msanii.