Mbasha akataa kutelekeza familia
Msanii wa nyimbo za injili nchini Tanzania Bwana Emmanuel Mbasha hivi karibuni alikutwa na kashfa iliyokuwa ikisambaa katika miatandao kuwa msanii huyo ametelekeza familia mbili tofauti (wanawake wawili tofauti kila mmoja akiwa na watoto) amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa tetesi hizo ni uongo, na hakuna kitu kama hicho na yeye hawezi kufanya hivyo,
Akiongea na mwandishi wa kituo cha televisheni cha EATV , Mbasha amesema kuwa ‘ si kweli hivyo vitu ni vya uongo ,nakanusha kabisa hivi kwanini vitu vinaongelewa vya uongo alafu mimi sipendagi ” anaongea Mbasha na kuonekana kukataa kabisa kuhusu tabia ya watu kuzushia mambo yasiyo ya kweli.Hata hivyo Mbasha anasema kuwa tabia ya kuzushazusha vitu ni kutafuta kiki na ni mambo ambayo yanafanywa na watu wa Bongo Fleva sio yeye muimbaji wa injili “huo uongo uongo ni tabia za Bongo Fleva , mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelewa vitu ambavyo havina faida ” aliongezea Mbasha.
Tetesi hizo zinazo endelea kuenea katika mitandao kwa kipindi cha hivi karibuni ni kuwa msanii huyu wa injili Emmanuel Mbasha amewzalisha wanawake wawili tofauti na kuwatelekeza na watoto wao nkisha yenyewe kujiingiza katika mahusiano na mwanamke mwingine inayesemekana kuwa yuko vizuri kifedha na ndiye anaemueka mjini msanii huyo.
Ni muda umepita sasa tangu Mbasha akabiliwe na kesi ya ubakaji, iliyomfanya kufikishwa mahakamani ambapo baaada ya hapo alishinda kesi iyo dhidi ya mkewe aliyemshitakia, mashataka hayo, baaada ya kesi iyo Mbasha aliingia katiak mgogoro mkubwa uliosababbisha yeye kuachana na mke wake na kupeana talaka , mke wa Emanuel Mbasha ,Florah Mbasha pia ni msanii mkubwa na mkongwe wa injili nchini Tanzania na kwa kipindi cha nyuma alitamba sana na vibao vyake kama ‘jipe moyo’ na ‘mwanamke simama imara’, wawili hao walipokuwa wakiachana tayari walikuwa wamepata watoto wawili na walikuwa wakifanya pamoja kazi za muziki .Hata hivyo baada ya talaka Florah Mbasha alifunga ndoa na mwanamke mwingine huku akibaki na watoto wao wawili,