Picha za Hamisa na Diamond zavuja
Ni zaidi ya mwaka sasa upite tangu kuwepo na tetesi za kuwepo kwa mahusiano kati ya msanii wa Bongo Fleva Diamond Platinumz na video queen maarufu wa Bongo Hamisa Mobeto.Hamisa ambae amekuwa akitishia uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na mzazi mwenzie na msanii huyo Zari The Bosylady,hata hivyo miezi michache iliyopita Hamisa alijifungua mtoto wa kiume aliempa jina la Prince Adbul Nasib au’ Tanzania baby’, mtoto ambae inasemekana kuwa ni mtoto wa Diamond Platinumz huku akiongeza idadi ya watoto wa msanii huyo mkubwa kuwa watatu .Tangu kuwepo kwa tetesi hizo Diamond mwenyewe amekuwa akikanusha tetesi hizo na kusema kuwa hana uhusiano wowote na video queen huyo ,zaidi ya mahusiano ya kikazi tena hasa walipokutana katika kushoot video ya wimbo wa ‘salome’ , wimbo ambao uliozua mambo mengi na ndipo tetesi za wawili hao kutoka ulipoanza kusambaa.
Zari , mama mzazi wa watoto wawili aliozaa na Diamond amekuwa akijikuta katika vita ya kimtandao na mashabiki na hata Hamisa mwenyewe huku sababu kubwa ikiwa ni kuwepo kwa tetesi hizo. Pamoja na hayo yote nata Hamisa mwenyewe amekuwa akirusha madongo hewani bila kudhibitisha moja kwa moja ukweli wa tetesi hizo.
Wapo mashabiki wanaosema kuwa wawili hao (Hamisa na Diamond ) wamekuwa wakionekana pamoja baadhi ya maeneo, lakini pia ukiachana na hayo, kipindi ambacho Hamisa Mobeto amejifungua wanafamilia wa Diamond walikuwa ni moja ya watu wa karibu walikwenda kumtembelea Hamisa hospitali ambapo alilazwa mrembo huyo.
Baada ya tetesi hizo kuwepo kwa muda sasa, zimevuja picha zinazosadikika kuwa ni picha za Diamond na Hamisa Mobeto wakiwa chumbani , huku mkono wa diamond wenye kuonyesha tatoo yake, hata hivyo picha zingine zinazoendelea kusambaa ni zile zinazimuonyesha Hamisa yupo kwenye chumba ambacho ni chumba cha kulala cha Diamond na mama watoto wake huku eneo ilo likionekana kufafanana kabisa na lile ambalo Zari amekuwa akipost picha katika ukurasa wake wa instagram kama sehemu yake ya kulala pia.