Fiesta Dar Kuhairishwa Masaa Machache Kabla ya Tamasha.

Lile tamasha lililokuwa linatarjiwa kufanyika wikiedi hii katika viwanja vya Leaders Club limevunjwa na hata kutofanyika tena kwa madai kuwa uwanja waliotaka kufanyia shughuli hiyo hauna sifa ya kufanyiwa shughuli hiyo.

Tamasha la Fiesta ambalo siku zote limekuwa likifanyikia Leaders club na mkoa wa Dar Es Salaam huwa ndio mkoa wa mwisho limevunjwa siku ya kilele ambayo ni tareh 24 asubui huku taarifa zikidai kuwa uongozi wa wilaya umewataka kuhamisha tamasha hilo katika viwanja vya Tanganyika Peakers ilhali walikuwa tayari walishaanda kila kitu mpaka majukwaa na hata wafanyabaishara walishajenga vibanda huko.

download latest music    

Tamasha hilo ambalo kwa sasa linaonekana kuingiwa na figusi nyingi ikiwemo maswala ya bifu baina ya pande mbili lilikufa bila watu kuamini kwa sababu ya maandalizi ya wasanii lakini pia mashabiki ambao walikuwa tayari walishajiandaa kwa kila kitu.

Kwa wale wanaolewa, utagundua kuwa tamasha hili ubeba watu wengi sana hivyo hata wafanya biashara ujipata wakitumia pesa nyingi kuandaa mazingira ya biashara kwa sabab wanategemea pia kurudsha faida kubwa sana lakini mwaka huu imewatia hasarawafanyabiashara.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.