Nandy Kupanda Steji Moja na Hamisa Mobetto
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ametangaza habari njema kwa mashabiki Wake wanaokaa nje ya nchi kwani anatarajiwa kupanda steji moja na Hamisa Mobetto.
Nandy ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Aibu’ ameweka wazi kuwa mwezi huu baadae anatarajia kuungana na Hamisa Mobetto kwa ajili ya your yake ya nchini Marekani.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Nandy ameweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Aslay wanatarajia kuungana na Hamisa Mobetto nchini Marekani.
Natarajia kusafiri siku ya tarehe 25 mwezi huu kuelekea Marekani kwa ajili yakufanya ziara nikiwa na msanii mwenzangu Aslay na Hamisa kisha nitarudi Bongo tarehe 10, Desemba tukiwa wote watatu, pia hii kwangu itakuwa ni mara ya kwanza kufika huko kwa sababu sijawahi kwenda kabisa”.
Hamisa Mobetto amekuwepo nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi sasa ambapo ameonekana akiwa anafanya matamasha katika majimbo mbali mbali katik nchi hiyo.