Diamond Ampangishia Hawa Hoteli Baada Ya Matibabu
Msanii aliyewahi kutamba kwenye kibao cha ‘Ntarejea’ Hawa Said amedaiwa kukaa kwenye hoteli aliyopangishiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Wiki chache zilizopita Diamond alitoa zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya matibabu ya mrembo Hawa ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya ugonjwa wa moyo.
Baada ya kumaliza matibabu na Kurudi nchini Tanzania, Hawa amepangishiwa hoteli ambapo atakaa kwa muda wa miezi mutate ili kuepusha usumbufu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, mama wa Hawa, Ndagina Kapera alithibitisha mtoto wake kurejea salama kutoka nchini India alikokuwa kimatibabu akiwa na afya ambapo baada ya kutua amepangishiwa chumba hotelini kwa ajili ya kuepusha usumbufu wa kelele.
Hawa amepewa masharti ya kukaa sehemu iliyotulia, isiyo na kelele kutokana na tatizo lake la moyo hivyo amepangishiwa hoteli moja hapa jijini Dar (jina linahifadhiwa) na meneja wa Wasafi (Hamis Taletale ‘Babu Tale’) kwa muda wa miezi mitatu mpaka afya yake itakapotengamaa“.
Mama huyo ameweka wazi shukrani zake za dhati kwa Msanii Diamond Platnumz kwa Kuokoa maisha ya Mtoto Wake.