“Siamini kama bff anaweza kunifanyia vitendo vibaya”-Wolper
Msanii wa Bongo Movies na mjasiriamali ambae amekuwa na skendo za hapa na pale mitandaoni lakini amekuwa akionesha kuzoea na kutokujali maneno ya watu Jackline Wolper ameongea na kufunguka kuwa mpenzi wake mpya aliyenae sasa hivi ambae pia ni mwanamitindo anaejulikana kwa jina la Brown ambae yeye Wolper amezoea kumuita ‘bff’ kuwa mwanaume huyo ndie mwanaume anaemuamini sana na anajua kuwa ni mwanaume wa tofauti kuliko wanaume aliowapitia hapo awali.
Wolper ambae alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize na kuachana hivi karibuni kwa kutupiana maneno katika mitandao alimsifia mpenzi wake huyo mpya na kusema kuwa kaka huyo ni mcha Mungu sana hivyo anaamini hawezi kufanya mambo mabaya kabisa kama kule alipotoka.
Ingawa wolper ameonekana kukiri kuwa katika mapenzi wanaume sio wa kuwaamini na wengi wana matendo ya kufanana, lakini anaamini bff wake hawezi kufanya mambo kama hayo.
“Siamini kama bff anaweza kunifanyia vitendo vibaya kama nilivyowahi kufanyiwa hapo awali .Namuamini sana kutokana na kuwa yeye ana hofu ya Mungu , lakini sisi bado ni binadamu,anaweza kunikosea kawaida au mimi nikamkosea hiyo ni kawaida kwa sababu sis ni binadamu hiyo haitanifanya nimchukie, lakini akifika huku pa kunifanya niumie kama nilikotoka nitaamini kuwa hakuna wa kumuaini tena katika mapenzi ” anasema Wolper.
Licha ya bifu zinazoendelea kati yake yeye na mpenzi wake wa zamani na kuumizwa na mwanaaume huyo kama anavyodai yeye mwenyewe lakini bado anaamini kabisa kuwa mwanaume aliyenae sasa ndie mwanaume aliyekuwa anamtaka na kumtafuta siku zote sababu ni mcha Mungu na ana heshima pia.
Ingawa kumekuwa na maneno mengi katika mitandao watu wakisema tangu awe na mahusiano na mwanaume huyo aliyenae sasa kuwa ni mdogo huku watu wakimuita Wolper ‘sugar mamy’, lakini kwake hajali maana anaamini kuwepo kwa mapenzi ya kweli kati yake na bff , hivyo kwa Wolper umri sio kigezo cha kumtenganisha na bff wake