Fid Q Atangaza Kufunga Ndoa Kabla Ya Mwaka Kuisha
Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu Kama Fid Q ameibuka na kuweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa mwaka huu Baadaye.
Fid Q ameweka wazi moja kati ya watu walimsukuma kufikia uamuzi huo ni Msanii mwenzake Stamina ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu.
Fid Q alifunguka hayo Wiki iliyopita kwenye sherehe fupi ya kumbu kumbu ya siku ya kuzaliwa Stamina, ambapo alieleza kuwa maisha ya ndoa yanambadilisha mtu.
Kitu ambacho hukifahamu wewe (STAMINA) au labda watu wengi hawakifahamu. Wewe pia unani-inspire mimi siku hizi unanielewa vizuri, Unani-inspire kama Artist, Lifestyle, umebadilika sana siku hizi umekuwa mtu wa familia. Kwa kupitia wewe mimi nina mpango wa kuoa mwezi Desemba”.
Fid Q na mpenzi wake huyo wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja.