Wema- Aunty Ndiye Rafiki Pekee Ambaye Hanichoki
Muigizaji wa filamu za Bongo movie Wema Sepetu amedai rafiki yake Aunty Ezekiel ndiye rafiki pekee ambaye amekuwa naye bega kwa bega Bila kuchoka katika hiko kipindi kigumu anachopitia.
Wiki chache zilizopita Wema Aliibua gumzo zito mara Baada ya kuachia video za faragha akiwa na mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii jambo lililomuingiza katika matatizo.
Wema Sepetu amefunguka na kudai rafiki yake wa kweli ni Aunt Ezekiel kwani hajawahi kumchoka na kumtenga kama wafanyavyo wengine na kusisitiza kuwa kuwa ana marafiki wengi lakini baadhi ni wanafiki ila Aunt ana upendo wa kweli kwake.
Nimegundua kuwa rafiki wa kweli kwangu ni Aunt, amenipa faraja ya kweli kipindi chote cha matatizo, naamini ana upendo na mimi”.
Baada ya kuingia katika sakata hilo wasanii kadhaa walimgeuka na kutaka apewe adhabu ambayo itamfanya asirudie makosa hayo huku wengine wakiwa Upande wake.