Duma na Gabo hali bado ni tete,waendelea kuchafuana.

Mfarakano unazidi kuwa mkubwa kati ya wasanii wa bongo movie kati ya Daudi Michael’Duma’ aliyepata  umaarufu katika tamthilia ya Siri ya Mtungi pamoja na msanii mwezie Gabo Zigamba, vita hiyo ilianza pale ambapo duma alianza kwa kumkashifu msanii mwezie kuwa hajui kuingiza na anaharibu tasnia hiyo,Duma anadai kuwa Gabo amekuwa ni mtu wa kuiua Bongo Movie na wala sio kuiendeleza kabisa

“Huyu jamaa ni kirusi katika tasnia yetu,angalia kwa mfano mpaka sasa ameshapokea tuzo kama nne lakini hakuna anachofanya,haeleweki anafanya nini , hata ukiomuona barabarani anapita huwezi kuamini kama  ni staa wa filamu nchini” anasema Duma

download latest music    

Duma pia anamponda Gabo kuwa hana umaridadi, “Gabo hana cha kuongea, hata watu wanamuogopa hawawezi kumuita  katika sherehe mbalimbali anarudi suti, zaidi ya mara tatu ,yaani yupoyupo tu, anauza sura haeleweki,yaani anaangusha watanzania”

Kwa upande wake Gabo alipoulizwa kuhusu maneno hayo Gabo alisema kuwa yeye hayuko tayari kuongea chochote maana Duma  ndio alieamua kumzungumzia, “sinaga urafiki  kwanza na mwanataaluma ambae tunafanana taaluma,ila upo ujamaa tu lakini maneno haya kwangu hayana nafasi..akili ukiweza kuitumia vizuri unaweza kufanya mabo mengi ya msingi ” aliongezea Gabo

Akiongea na Times Fm , Duma anajaribu kujitetea na kusema kuwa watanzaania wamekuwa wakishikilia maneno machache tu, lakini yeye anapomuongelea Gabo anaangalia jinsi ambavyo Gabo hajawahi hata kufanya filamu nje ya Tanzania  wala kufanya muvi  za kimataifa lakini bado watanzania wanamuamini,lakini pia tangu mwaka huu uanze hajawai kutoa filamu yoyote,ivyo anawaangusha mashabiki zake ambao wamekuwa wakimuamini na kumpenda na ndio mwishoni inasemekana kuwa watu wa filamu wamepotea.Duma anaamini kuwa mashabiki wanamuamini sana ivyo Gabo anapaswa kufanya vitu ili kuendelea kuwaaminisha mashabiki,anapokaa kimya na kusgindwa kufanya chochote inaonekana bongo movie imelala, ivyo Gabo inabidi aamke ili kuendeleza tasnia ya filamu.

Anasema hawezi kuwaongelewa watu kama Steve Nyerere au Ray kwa sababu hao tayari ni watu wakubwa katika tasnia, ila anajitaidi kuangalia hawa waliopo katika usawa wake.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.