Diamond ,Vannessa,Alikiba kuwakilisha Tanzania tuzo za MEAMA
Wasanii Diamond, Vannessa pamoja na Alikiba wamechaguliwa kuwania katika tuzo za Middle East Africa Music Award (MEAMA) ,tuzo hizo ambazo zinapangwa kufanyika tarhe 5 Oktoba mwaka hu zina lengo la kuibua vipaji na kuonyesha amasa kwa wasanii wa africa kwa ujumla.Akiongea katika uzinduzi wa tuzo hizo kwa awamu ya pili CEO wa FAJ GLOBAL ENT.L.T.D ,MAJESTICAL ROYAL CLUB (MRC) na pia ni mwenyekiti wa FAJ ONLINE-RADIO Mr. Fajuyi Adeniyi Oluwaseun amesema kwamba wanaahidi kuwa kwa mwaka huu tuzo izo zitakuwa zenye ubunifu zaidi na zina kuwa na lengo la kuibua vipaji vingi zaidi ili kuendelea kuipa sifa na kuitangaza Africa.
Tuzo hizo ambazo zimejumuisha washiriki wengi ambao wametoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya,Uganda, Nigeria, South Sudan,Tanzania, Egypt na zinginezo jana tarehe 13 Septemba imeelekezwa kuwa majina ya washiriki kutoka nchi zote yanapatikana katika website ya tuzo hizo hivyo mashabiki waweze kuwapigia kura wasanii wao wanaowapenda ili waweze kujinyakulia tuzo izo.
Kwa upande wa Tanzania msanii wa kike Vannesa Mdee ndiye msanii pekee wa kike kutoka nchini hapa aliyewekwa katika kategoria ya msanii bora wa kike wa mwaka huku akichuana na Victoria Kimani,Yemi Arade na Seyi Shayi, kwa upande wa wanaume yupo alikiba katika kategoria ya msanii bora wa kium wa mwaka,pamoja na Diamond Platinumz katika kategoria ya wimbo bora ya mwaka na wimbo wa Eneka .
Wasanii wengine wanaoshiriki kuwania tuzo izo kutaka nchi tofauti na Tanzania ni pamoja na Davido,Wizkid,Mr.Eazi katika kategoria tofauti tofauti.
Mashabiki wanahamasishwa kupigia kura msanii anaependa kushinda katika tuzo izo,na jinsi ya kupiga kula ni kuingia moja kwa moja katika website ya tuzo izo (MEAMA) ambapo upigaji wa kula umeanza mara baada ya kutangazwa kwa washiriki huku mwisho wa kupiga kula ikiwa ni tarehe 30 septemba mwaka huu na tuzo kufanyika oktoba 5 nchi Egypt.Tunawatakia mema wasanii wote waliopo katika kategoria mbalimbali , muziki wa Africa unafika mbali kwa sasa.