Shilole Afungukia Mkosi Wa Nyumba Yake Mpya
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa baada ya kuhamia kwenye mjengo wake mpya lakini amekiri kukaribishwa na mkosi.
Global Publishers wanaripoti kuwa Shilole alitokelezea kwenye uzinduzi wa Albamu ya Nandy lakini Ghafla aliibua minong’ono Baada ya kuonekana na nundu usoni hali iiyopelekea watu kudhani huenda Mumewe Uchebe amemtembezea kichapo.
Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Shilole alifunguka na kusema:
Aaa…Unajua juzijuzi ndiyo nimehamia nyumbani kwangu Majohe, sasa nyumba yenyewe bado sijaizoea na bado sijaweka umeme, sasa niliporudi usiku nikiwa nimechoka ndiyo nikajikuta napiga mwereka na kuumia hivi.
Si unajua nyumba usiyoizoea? Hayo ndiyo yaliyonikuta na hii pati kwa kuwa nilishaalikwa na kumhakikishia Nandy kuwa nitakuwepo, nimeona nijikongoje nifike haina jinsi”.
Miezi michache iliyopita Shilole alianika mjengo Wake mpya alioujenga kwa kutumia pesa aliyopata kupitia Sanaa na biashara zake.