Sanchi Aanika Siri Nyuma Ya Msambwanda Wake
Mrembo anayekimbuza hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi Siri ya kuwa na shepu Kama yake.
Kwenye interview yake na Gazeti la Risasi Jumamosi, Sanchi alisema kuwa, madafu yana mchango mkubwa sana kwenye shepu yake kwani hupendelea kunywa maji yake badala ya maji ya kawaida au kimiminika kingine.
Mimi nitawapa siri yangu leo, madafu ndio kila kitu kwangu na hii tangu niko mdogo. Mama alikuwa akipenda sana kunywa maji ya madafu, nikawa namuuliza kwanini.
Lakini pia Sanchi anaweka wazi kuwa maji ya madafu yanafanya tumbo kuwa na mfumo mzuri kwa sababu yanasafisha kila kitu, hadi mkojo unakuwa safi.
Kuanzia wakati huo kila nikisikia kiu, labda dafu lisiwepo lakini likiwa lipo karibu maji yake ndiyo ya kuniondolea kiu, najua pia yananifanya nionekane mrembo zaidi”.
Sanchi amefunguka hayo Baada ya Kuwepo kwa tetesi kuwa umbo hilo matata alilokuwa nalo huenda likawa ni fekero jambo ambalo amelikana na kuweka wazi kuwa mama yake mzazi amejaaliwa msambwanda Kama Wake.