“Nafarijika Kuona Unatabasamu Sasa”-Diamond Platnumz
Msanii wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa WCB Abdul Naseb maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka kuhusu matibabu ya msanii mwenzake Hawa Said.
Mwezi uliopita Diamond alitangaza kumpeleka Hawa nchini India kwa ajili ya matibabu ambapo alipofika alikutwa na ugonjwa wa moyo na kufanyiwa upasuaji.
Siku ya Leo meneja wa Diamond, Babu Tale aliweka wazi kuwa Mpaka sasa Hawa anaendelea vizuri na Ana afya njema kabisa Baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka wazi furaha yake Baada ya kuona afya ya Hawa imeimarika Lakini pia ameweka wazi hatomuacha mikono mitupu akisharudi Tanzania kwani amemtaka atafute biashara ya kufanya na yeye atamsaidia mtaji.