Nandy Amtaja Aslay Kama Msanii Alimtungia Nyimbo Kwa Ajili Ya Albamu Yake
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini kutoka katika Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Faustina Charles maarufu kama Nandy amefungukia Albamu yake mpya.
Albamu mpya ya Nandy ambayo hivi sasa iko sokoni inaitwa ‘The African Princess” Kiowa ni albamu yake ya kwanza kuingiza sokoni tangu aanze Sanaa yake ya kimuziki.
Nandy ameweka wazi kuwa Albamu hiyo imemchukua Kama mwaka mzima kuiandaaa tu huku nyimbo zake akiandikiwa na msanii Kama Jay Melody na staa mkubwa wa Bongo fleva Aslay.
Kusema ukweli Albamu yangu imechukua muda mrefu kukamilika kwa sababu nimekuwa nikitungiwa nyimbo na wasanii Kama Aslay na Jay Melody”.
Kwneye mahojino na kituo kimoja cha habari Nandy amefunguka haya kuhusu muziki wake na albamu yake hiyo:
Imenichukua mwaka mzima kutengeneza albamu yangu ili kupata Kitu kizuri hii imekuwa kwa sababu ya kusafiri kwa ajili ya kufanya shoo mbali mbali ambazo zimechukua muda wangu mwingi”.