Zari Atangaza Zawadi Kwa Mashabiki Zake Uganda
Mwanamama mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda na Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ ametoa zawadi Nono kwa mashabiki zake nchini Uganda.
Zari ameyafanya hayo muda mfupi baada ya kupata zali la kuwepo katika vivutio vikubwa vya utalii nchini humo akiwa kama balozi wa utalii ambapo atatembelea katika mbuga kubwa za wanyama pamoja na chanzo cha Mto Nile pande za Jinja.
Akizungumzia ishu hiyo ndani ya Hoteli ya Serena nchini Uganda, Zari alisema ili kuwavutia watalii na watu wengine ameona kuwa na kampeni maalum ya kuwashirikisha mashabiki wake na kampeni hiyo ameiita jina la Tulambule Ne Zari akimaanisha Tutembee Na Zari.
Niambie sehemu unayopenda kutembelea Uganda, unaweza ‘ku-google’ vivutio vyote vya utalii Uganda na ukasema ni sehemu gani unapenda kutembelea,” alisema Zari na kuongeza: “Nitatoa ofa ya gharama zote za safari na ujue tu mimi ni Boss Lady kwako na kwa mwenzako au familia yako”.
Hili ni moja tu Kati ya madili ambayo Zari amekuwa akiyapiga tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz Lakini pia Kumekuwa na tetesi za ubalozi wa nchi unaoweza kumuangukia mrembo huyo.