Hamisa Mobetto Amuanika Mpenzi Wake Mpya (video)
Mwanamitindo na msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto kwa Mara ya kwanza ameanika video zinazomuonyesha akiwa na mwanaume ambaye anasemekana kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Hamisa ambaye hivi sasa yupo nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki ameonekana kupata na penzi jipya kwani ameweka video zinazomuonyesha akiwa na Kijana mwingine huku wakiwa wameshikana mikono na hata baadhi ya video zimewaonyesha wakiwa wamebebana.
https://www.instagram.com/p/Bp6KT4YB095/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=s07nf6psfruv
Mpaka sasa Hamisa hajatoa tamko lolote kuhusu uhusiano wake na kijana huyo lakini picha na video zimejieleza kuwa inawezekana akawa mtu wa kuziba pengo la Baba watoto wake Diamond Platnumz.