Shamsa Ford Akiri Kusumbuliwa na Wapenzi Wa Zamani Wa Chiddi Mapenzi
Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Shamsa Ford amefunguka na kudai anapata sana usumbufu kutoka kwa Wanamaker ambao wamewahi kuwa wapenzi wa mume wake Chiddi Mapenzi.
Shamsa amedai usumbufu ambao amekuwa akikumbana nao ni mkubwa sana kwani wamekuwa wakimfanyia visa yeye kwa wivu kwa kuwa yeye ndio mke halali wa ndoa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shamsa alisema amekuwa akisumbuliwa na wanawake ambao waliwahi kutoka kimapenzi na mumewe ambapo kila anapokutana nao wamekuwa wakimfanyia visa kama kumpiga vikumbo na fujo nyingine za hapa na pale.
Kiukweli wanawake wa zamani wa mume wangu wananisumbua sana, kila ninapokutana nao wananipiga vikumbo, wananifanyia visa na maneno kibao yakiwatoka huku wakitaja jina la Chid, naomba niwaambie tu kuwa wanatakiwa kukubaliana na hali halisi maana aliniona ninamfaa ndiyo akanioa na kuniweka ndani hivyo fujo wanazofanya hazisaidii bali wanatakiwa watafute wa kwao”.