Babu Tale-Tumeshaanza Kuwasiliana na Uongozi Wa Ali Kiba
Meneja wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi mipango yao ya kumpata msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival.
Siku ya Jana kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz aliweka wazi mipango yao ya kumpata Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye shoo yao.
Lakini sasa Meneja wa Diamond Babu Tale anafunguka kuhusu jitihada zao za kuwasiliana na Kiba ambapo amekiri kuwa hana mawasiliano na Kiba lakini anaelewana sana na meneja wake anayeitwa Seven.
Siongeagi na Alikiba kivile, mimi naongeaga na meneja wake maana alishawahi kunisaidia sana, lakini kuhusu inshu ya Wasafi Festival Sallam ameshaanza kuwasiliana na uongozi wa Alikiba”.
Baby Tale ameweka wazi kuwa siku ya uzinduzi wa Wasafi festival pamoja na wasafi fm mbali ya kuwepo kwa mipango ya kumpata Ali Kiba lakini pjs atakuwepo msanii Konki konki konki master Dudu baya katika tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Wasafi media.