Mchekeshaji Mc Pilipili apata ajali ya gari
Mchekeshaji maarufu nchi Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili jana tarehe 12 septemba alipata ajali ya gari katika barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza.Mchekeshaji huyo ambae kwenye gari w alikuwa na watu wengine wawili na yeye watatu huku dereva akijulikana kwa jina la Said Hassan. Ilielezwa kuwa gari aina ya Prado ndio lililohusika kwenye ajali iyo maeneo ya Bubiki mkoani Shinyanga na watu wote walikimbizwa haraka sana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza.
Hata hivyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Shinyanga kamanda wa polisi mkoani humo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema kuwa chanzo cha ajali aliyoipata Mc Pilipili na wenzie ni kuwa alikuwa anamkwepa mtoto mdogo aliyekuwa akiendesha baiskeli lakini pia dereva ya gari hiyo alikuwa katika mwendokasi,katika kuelezea ajali iyo kama huyo anasema kuwa gari iliacha njia na kupinduka .mc pilipili amepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwa ni pamoja na sehemu za kifua.Kwa upande wa dereva aliumia sehemu za mkononi ,mkono wa kulia na majeraha wote wapo hospitali hapo kwa matitababu zaidi .
Akiongea na mwandishi wa gazeti la mwananchi,Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo ili kuelezea hali yake alisema kuwa ni kweli wamempokea katika kitengo cha dharura na amehudumiwa, hali yake bado haijaimarika na kwa sasa Mc Pilipili yupo chumba cha wagonjwa wanaitaji uangalizi zaidi huku wakiendelea kumfanyia vipimo vingine.
Inaelezwa kuwa mc pilipili alipata ajali iyo alipokuwa anatoka Shinyanga kwenda Mwanza ambapo alikuwa amearikwa katika kusherekea harusi mkoani humu,
Kwa kudhiirisha taarifa hizo wasanii na watu mbalimbali katika tasnia yake wamekuwa wakiposti picha katika kurasa zao za instagram za mchekeshaji huyo maarufu huku wakimtakia apone haraka na wengine wakimpa pole kwa kupata ajali, lakini pia baadhi yao pia wameonekana wakitoka hospitali kumjulia hali ikiwepo Belle 9, na Katarina Karatu ambao walipata bahati ya kwenda kumjulia hali.Tunamtaki Mc Pilipili afya njema na apone haraka.