Msanii Irene Mwamfupe Kufanya Uzinduzi Mkubwa Wa Albamu Yake
Msanii wa nyimbo za injili Irene Mwamfupe ametangaza kufanya uzinduzi mkubwa wa albamu yake itakayoitwa ‘Hodari’.
Uzinduzi huo utafanyika Novemba 25, mwaka huu na kupambwa na waimbaji wakubwa Injili akiwemo Bahati Bukuku, Happy Milinga, Mariam Kilyenyi, Martha Mwaipaja, Bony Mwaitege na Edda Mwampanga.
Akiuzungumzia uzinduzi huo utakaofanyika ndani ya Kanisa la Mito ya Baraka, Kariakoo jiini Dar, Irene alisema siku hiyo ambayo ni Jumapili, itakuwa ya kumsifu Mungu na kupokea miujiza kupitia sifa.
Niwakaribishe watu wote, hakutakuwa na kiingilio, waje washuhudie uzinduzi wa albam yangu ya Hodari na pia wataweza kuwasikia na kuwaona wanamuziki wenzangu wa muziki wa Injili’.
rene alisema mbali na waimbaji hao, waimbaji wengine watakaoupamba uzinduzi wake ni pamoja na Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Emmanuel Mbasha, Madam Ruth, Happy Mlinga, Edda Mwampagama na kwaya zote za Mito ya Baraka ambazo ni Jerusalem Choir, Rehema Kwaya, Ebenezer Kwaya, WWI Kwaya na The Joshua Generation.