Kajala-Umri Umenikatisha Tamaa Ya Kuzaa Mtoto Mwingine
Msanii wa filamu za Bongo movie na mtangazaji na balozi wa Biko, Kajala Masanja ameibuka na kuweka wazi kuwa amekata tamaa ya kuzaa mtoto mwingine kutokana na umri wake kumtupa mkono.
Kwenye mahojiano na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Kajala amesema kuwa, kipindi cha nyuma alikuwa akisaka mtoto mno, lakini ilishindikana hivyo umri unasogea na pia mtoto wake ameshakua ni msichana mkubwa hivyo inabidi aangalie maisha mengine na siyo kuzaa tena.
Nilitamani sana kupata hata watoto wawili, lakini ilishindikana kwa wakati, hivyo nimeona bora sasa kuangalia kitu kingine mbele maana nimekata tamaa kabisa ya kuongeza mtoto mwingine, ninajikita kwenye kumuwezeshe Paula asonge mbele kielimu”.
Kajala ameweka wazi kuwa kwa sasa ana umri wa miaka 36 hivyo anajiona tayari ameshakuwa mtu mzima sana. Kajala amezaa mtoto mmoja na mtayarishaji legendari wa muziki wa Bongo fleva P funk Majani.