Mbasha Azidi Kumchokonoa Mc Pilipili
Msanii wa nyimbo za Injili nchini Emmanuel Mbasha ameibuka na kumtupia madongo Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ baada ya kupiga picha akiwa na mpenzi wake.
Siku chache zilizopita Mc Pilipili aliposti picha Mtandaoni akiwa na mpenzi wake anajulikana kama Qute Mena lakini mara moja Mbasha alimtolea povu Mc Pilipili na kudai kwa kufanya hivyo amekiuka taratibu za kidini.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mbasha alisema lengo la kumuandikia ujumbe mrefu MC Pilipili kwenye ukurasa wake wa Instagram, lilikuwa ni kumjenga pamoja na kumuelimisha kwamba kitendo anachokifanya sio sahihi.
Unajua sio vizuri kumuanika wazi wazi mchumba wala kuwa naye karibu kiasi ambacho hata watu wakiwaona watashangaa, kwa sababu tunafundishwa kwamba, ukishamchumbia mtoto wa kike hutakiwi kufanya naye kitu chochote mpaka pale utakapo muoa na kumfanya mke wako.
Sasa Napata wasiwasi kwa huyu ndugu yangu MC Pilipili na huyo mchumba wake, nimepata taarifa kwamba wapo Zanzibar sasa sijajua kama wamechukua vyumba tofauti au wanaishi kwenye chumba kimoja, kitendo ambacho si kizuri, ila lengo la kumuandikia ule ujumbe kwenye akaunti yangu ni kumuelisha kwa sababu yeye ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza kutoka kwake”.