Nandy Azima Tetesi Za Kuwa Mjamzito
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kukataa kata kata tetesi zilizombaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa hivi sasa ni mjamzito.
Nandy ambaye hivi sasa anafanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Aibu’ amekataa tetesi za kuwa hivi sasa amejazwa kibendi na Kigogo mmoja na kudai ni uzushi tu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy alisema watu huwa wanaamua tu kuzusha mambo yasiyokuwa na ukweli wowote ule ndani yake, ili mradi tu wafurahishe mioyo yao kitu ambacho kinaumiza.
Hizo tetesi zinazosambaa mitandaoni kwamba nina mimba siyo za kweli, ila naona watu wameamua tu kuzizusha ili wafurahishe mioyo yao, sina mimba jamani naomba waniache“.