Rapa Wakazi Kupita Njia za Nandy
Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana (Rap) Wakazi ameweka wazi nia yake ya kufanya remix ya ngoma ya Msanii wa Bongo fleva Nandy.
Wakazi ameweka wazi kuwa yupo mbioni kutoa remix ya wimbo wa Nandy unaokwenda kwa jina la Aibu ambao unafanya vizuri kwa sasa kwenye chati mbalimbali za redio.
Siku za nyuma Utakumbuka Wakazi alifanya hivyo pia kwenye wimbo, Sijutii wa muimbaji Ruby ambaye anatajwa kuwa hasimu mkubwa na Nandy kimuziki kwa sasa. Pia Wakazi aliwahi kufanya refix ya wimbo wa msanii kutokea nchini Nigeria, Wizkid unaokwenda kwa jina laOjuelegba na kuipa jina la Natokea Dar .