Wema Sepetu Adai Hana Mpango Wa Kumuacha Mpenzi Wake
Muigizaji wa Bongo movie staa Wema Sepetu amefunguka na kusema pamoja na mashabiki wake kutokwa na povu zito baada ya yeye kumuanika mpenzi wake lakini yeye ndio amemchagua.
Wiki iliyopita Wema alizua gumzo baada ya kuanika picha Mtandaoni akiwa na mpenzi wake amayejulikna kama Patrick Christopher ‘PCK’ ambapo mashabiki zake wengi walionekana kuchukizwa na Mahusiano hayo.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema amesema kuwa yeye ana uamuzi wake binafsi wa kufanya anachotaka kwenye maisha yake, lakini anashangaa watu wengine wanamuingilia mpaka kwenye maisha yake binafsi na kutokwa povu.
Yaani watu wametokwa na povu kama lote, kisa tu mimi kumuonesha mwanaume wangu, sasa hata wakiungana dunia nzima kunisema, kama nimeshampenda watanibadilisha vipi“.
Watu wengi wamejitokeza na kumshauri Wema aachane na yule mwanaume kwani haendani naye hata kidogo jambo ambalo limeonekana kumkera Wema.