Ray C Aanika Majibu Yake Ya Ukimwi
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameanika majibu yake ya kipimo cha virusi vya Ukimwi alichofanya siku za hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Msanii huyo ameweka majibu ya kipimo hiko kinachoonyesha hana maambukizo ya gonjea hilo la Ukimwi.
https://www.instagram.com/p/BpCTiygHEE1/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=w5cqoijgcq
Lakini pia amewaasa na watu wengine waende kupima ili kupata kujua majibu ya afya zao kwa ujumla.
Baada ya kimya kirefu kutokana na athari za matumizi ya madawa ya kulevya, Ray C ambaye kwa hivi sasa anaishi nchini Kenya na kuonekana katika nchi za Ughaibuni na mpenzi wake mzungu ametoa wimbo mpya unaoitwa ‘My woman’.