Chuchu Hansy Adai Yeye na Ray Tayari ni Kama Mume na Mke
Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ameibuka na kudai kuwa yeye na mzazi mwenzake staa wa Bongo movie Vicent Kigosi ‘Ray’ kisheria tayari ni mume na Mke bado tu kufanya sherehe.
Kwenye mahojiano yake na gazeti Amani, Chuchu alisema kuwa japokuwa wao na Ray wamezaa lakini wamekuwa ni kama marafiki sana na watu wanaoelewana hivyo imebaki tu sherehe.
Unajua mimi na Ray hatujaamua kuweka wazi tu au tufanye sherehe kwa sababu tumekaa pamoja muda mrefu sana yaani kisheria ni mke na mume hapa kwa mujibu wa sheria, siwezi kusema sherehe ni lini lakini wasubiri”.
Ray na Chuchu wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka mingi na kufanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden.