Wema Amuanika Hadharani Mpenzi Wake Mpya
Muigizaji wa Bongo movie supastaa Wema Sepetu amemuanika hadharani mwanaume ambaye yupo naye Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa sasa.
Wema alizua gumzo zito baada ya kumposti mwanaume huyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘My future husband’ akimaanisha mume wangu mtarajiwa.
Wema amekaa muda mrefu bila watu kumtambulisha mwanaume wake kwani alishazoea kuwapost wanaume anaokuwa nao kwenye mahusiano,kipindi cha hapa katikati watu walihisi mrembo huyo yupo kwenye mahusiano na muigizaji kutoka nchini Ghana ambaye amefanya nae Movie waliyoitambulisha mwezi wa tisa ambayo inajulikana kwa jina la D.A.D, na maswali hayo aliulizwa kwenye mahojiano yake mbalimbali na vyombo tofauti vya habari ila wema alikataa lakini leo ameweza kumuweka hadharani mwanaume wake.
Lakini pia mwanaume huyo ameonekana akikomenti Kwenye page ya Diamond na kumpa taarifa ndoa yake na Wema inafanyika tarehe 25.