Jux Ajibu Tuhuma Za Kumdhulumu Chid Benz
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux ameibuka na kujibu tuhuma nzito alizotupiwa na msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Chid Benz alipodai kuwa amemdhulumu pesa alizopigia shoo.
Siku chache zilizopita Chid Benz alimtuhumu Jux kwa utapeli baada ya kudai kuwa aliperfom Kwenye shoo ya ‘In Love and Money Tour’ lakini hakumlipa hata senti pamoja na kwamba mashabiki waliikubali shoo yake zaidi.
Katika mahojiano yake na Enews ya EATV, Jux amefunguka na kudai kuwa Chid hakuwepo Kwenye listi ya wasanii ambao walitakiwa kuperfom bali alimfuata backstage:
Kwanza kabisa Chid Benz hanidai pesa yoyote kwa sababu ile Show kabla hata ya kufika Dar tulikuwa tumeshapanga wasanii watakaotumbuiza hatukuwa na mdhamini kwaiyo hata wale wasanii waliotumbuiza Kuna vitu tuliwafanyia lakini hatukuwalipa hela na wengine walikuja kutusapoti tu kama wasanii wenzao.
Chid alinifuata backstage akasema anataka kufanya kitu kwa mashabiki na mimi nikamuheshimu kama braza mkubwa akapanda stejini akapiga shoo lakini kesho yake ananipigia simu ananiambia amelogwa shoo lakini hajapata kitu nikamwambia nitampa kitu kutoka mfukoni kwangu lakini haikuwa lazima nashangaa ameenda Kwenye vyombo vya habari”.