Naj Azima Tetesi Za Kuachana na Barakah The Prince
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Naj Dattan amezima tetesi za kufa kwa Penzi lake na msanii wa Mwenzake Barakah The Prince.
Siku ya jana kuna taarifa zilisambaa kwamba Penzi kati ya Naj na Barakah limeisha baada ya Msanii huyo kutoa kauli yenye utata kuhusu Penzi lao pale alipoulizwa kama wapo wote.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kwamba Naj amemmwaga Barakah kutokana na kuwepo kwa taarifa za michepuko na hata kusemekana kwamba Baraka amemjaza mimba binti mwingine.
Naj ameibuka na kuzima tetesi hizo kwa kuposti picha yake na Barakah na kuandika maneno ya kimahaba kuashiria kwamba Penzi lao halijafa kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa: