Nilianza Muziki Pamoja na Ali Kiba na Diamond-Tiko
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Mrembo Tiko Hassan maarufu kama Tiko amefunguka na kuweka wazi alianza muziki miaka ya nyuma pamoja na mastaa Ali Kiba na Diamond.
Tiko alijizolea umaarufu kwa mara ya kwanza kupitia kuigiza filamu za Bongo Movie lakini baada alihamia Kwenye upande wa Bongo fleva.
Kwenye mahojiano yake na Risasi Vibes , Tiko anasema kuwa ameanza sanaa siku nyingi sana tangu enzi hizo akiwa na akina Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Kiba ‘King Kiba’ walipokuwa wakihangaika ili kufikia malengo.
Mwaka ambao nilikuwa na wasanii wenzangu kama vile Diamond, Kiba na Queen Darleen zipo nyimbo ambazo nilitoa na pia nakumbuka Bob Junior alinipa nyimbo niliimba imba lakini sikufika mbali nikakutana na mtu akaniingiza kwenye filamu nikaenda huko “.
Tiki amesisitiza kuwa amejipanga kufanya vizuri zaidi ya alivyofanya miaka ya nyuma kwani angekomaa kama Wasanii Wenzake kama Diamond na Ali Kiba basi angeweza kuwa mbali kama wao.