“Usikubali Kuwa Mtumwa Wa Mapenzi”- Uwoya
Msanii wa Bongo movie Mrembo Irene Uwoya amefunguka kwa kutoa ujumbe mzito wa Kimapenzi na kuwasaidia watu wasikubali kugeuzwa watumwa wa mapenzi.
Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja wamekuwa wakitrend sana Kwenye mitandao ya kijamii na tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao na siku ya jana Uwoya kufichua kwamba mume wake huyo amewahi kuchepuka Kwenye ndoa yao.
Siku ya jana Uwoya ameibua maswali mengi mara baada ya kuweka ujumbe Kwenye ukurasa wake wa Instagram ulioibua maswali na kuonekana kama ni dongo kwa ndoa yake mwenyewe.