Nimenunua Kwa Pesa Yangu Kiwanja Cha Milioni 97-Sanchi
Socialite maarufu Janey Rimoy ‘Sanchi’ aliyejizlea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata na picha zake za utata amefunguka na kuanika kiwanja alichonunua kwa shilingi milioni 97.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sanchi ameweka wazi kuwa alimtumia kiwanja kile kwa pesa yake mwenyewe miaka michache iliyopita ba hata kudokeza kuwa anataka kuporomosha mjengo.
Sanchi amedai yeye ndiye kumiliki halali wa kiwanja kile ambacho kina ukubwa wa hekari kadhaa na kudai ana mpango wa kuporomosha Mjengo mara tu atakapomaliza kujenga nyumba yake ya sasa.
Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Sanchi aliweka wazi kuwa kiwanja kile ni muunganiko wa viwanja viwili na bei yake ni Milioni 97.