“Msimamo Kwenye Maisha Ndio Kila Kitu”- Odama
Msanii wa filamu za Bongo Movie Jennifer Kyaka maarufu kwa Jina la usanii kama Odama amefunguka na kuweka wazi msimamo wake ambao anao Kwenye maisha.
Odama amesema kuwa siku zote amekuwa mtu mwenye msimamo na kusimamia jambo lake, lakini anapofanya hivyo watu wanamchukulia tofauti na kumuona kama anaringa na asiyependa kusikia mtu na hicho ndicho kinamponza.
Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Odama amefunguka kuwa amejifunza kitu kikubwa kwenye maisha kupitia mama yake mzazi kwamba, kuwa na msimamo ndicho kitu muhimu kwenye maisha na ndicho anachofanya na hadi sasa amefanikiwa katika mambo yake mengi.
Kikubwa ni kuwa na msimamo katika mambo yako mengi ndiyo unaweza kusonga mbele zaidi na siyo vinginevyo. Ndiyo maana watu wengi wananiona tofauti kama ninaringa na nisiyependa kusikia cha mtu mwingine kumbe ni msimamo wangu tu ndiyo unaniponza nionekane hivyo“.