Esma Platnumz-Siwezi Tena Kumshauri Mama Yangu
Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan maarufu kama Esma Platnumz amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi Tena kuwa mshauri wa mama yake Bi Sandra maarufu kama Mama Diamond.
Familia ya Diamond inafahamika sana Kwenye mitandao ya kijamii kwa kupendelea kuanika mambo yao Kwenye mitandao ya kijamii lakini sasa Esma amepasua kuwa yeye ndiye alikuwa mshauri mkubwa wa Mama yake.
Kwenye mahojiano na Global Publishers, Esma ameweka wazi kuwa kwa sasa amestaafu rasmi kumpa ushauri mama yake kwani nafasi hiyo imezibwa na Baba yake wa kambo.
Nilikuwa ninampa ushauri kama mwanaye maana mimi ndiye mtoto wake mkubwa, lakini kwa sasa mama ana mume wake ambaye ni Anko Shamte kwa hiyo ndiye mshauri wake, sisi tunakaa pembeni”.