BASATA Inashusha Muziki Wa Bongo Fleva- Ben Paul
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini anayefanya miondoko ya RnB, Bernard Paul jina la usanii Ben Pol ameitupia lawama BASATA kama chanzo cha kushuka kwa muziki wa Bongo fleva.
Ben Pol amedai muziki wa Bongo fleva unashuka kutokana na presha kubwa ambayo wasanii wanapata kutoka kwa taasisi zinazosimamia muziki huu yaani BASATA.
Kwenye mahojiano na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Ben Pol amefunguka kama ifuatavyo:
Bongo Fleva na yenyewe kama imetetereka hapa katikati, naona kama kuna presha ya kutoa muziki mzuri, kuna presha ya kuwa relevant, kuna presha ya wasanii wachanga kutoka, kuna presha ya vyombo kama taasisi kumekuwa na presha ambao ndio walezi wetu.
BASATA ni chombo na chombo pia kinaongozwa na binadmu, hata tukikataa hatuwezi kujikataa kuwa sisi ni binadamu wote sisi ni binadamu. Kunaweza kuwa na makosa ya kibinadamu pia taasisi yoyote au chombo chochote kwa sababu kinaongozwa na binadamu kinaweza kikawa na makosa ya kibinadamu. Naheshimu namna ambavyo wanasimamia na wanapigania sanaa yetu lakini sote ni binadamu”.
Wasanii wengi wamekuwa wakiilaumu BASATA kwa kuwawekea vikwazo katika kutengeneza muziki mzuri kutokana na sheria mbali mbali.