Bahati Bukuku Akumbwa na Skendo Ya Utapeli Kongo

Msanii  wa muziki wa Injili Bahati Bukuku amejikuta katika wakati mgumu hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kuwa ni tapeli baada ya kudaiwa kulipwa pesa kwa ajili ya kufanya shoo nchini Congo lakini hakufika.

Global Publishers wanaripoti kuwa Bahati alitakiwa kwenda kufanya tamasha kwenye mkutano wa Injili ulioandaliwa na Askofu Wamwabi Francine wa Kanisa la Mlima wa Ushindi Mei, mwaka huu lakini hakutokea.

download latest music    

Gazeti la Amani lilifanya jitihada za kumtafuta Mwenyekiti wa Baraza la Wanamuziki lililopo Bukavu nchini Kongo, Wato Mukambilwa Adam ambaye alisema wamepokea malalamiko hayo na kuwasiliana na viongozi wa wanamuziki wa Injili Bongo.

Aliendelea kueleza kwamba, Askofu Wamwabi kupitia kwa Askofu Ben Cale

aliyemuunganisha na Bahati Bukuku alikuwa ameandaa mkutano ambao ulifanyika Mei, mwaka huu na walielewana kwamba malipo yake ni dola 2000 (zaidi ya shilingi milioni 4.5).

Alisema, baada ya kuelewana alitumiwa advansi kwa njia ya Western Union ambayo ni dola 1000 zilizobaki kutokana na mkataba walikubaliana kumalizana baadaye.

Siku ya mkutano ikiwa imekaribia, Bahati akawa anapigiwa simu ili kuambiwa kwamba anatumiwa tiketi ya ndege lakini simu yake hiyo ya mkononi ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa licha ya kutafutwa mara kadha wa kadha.

Mkutano ulifanyika na watu walikasirishwa sana kuona walivyotangaziwa kwamba Bahati atakuwepo walidanganywa, kitendo hicho kilimuudhi Askofu Wamwabi na kueleza ukweli kwamba mwimbaji huyo alimtapeli.

Askofu Wamwabi alieleza kwamba alifanya uchunguzi wake na kujua kuwa Bahati amemtapeli na siyo kwamba alikosa ndege kama alivyokuja kujitetea baadaye”.

Bahati Bukuku amelogwa marufuku Hingis nchini Congo kutokana na taarifa hizo za utapeli.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.