Kajala Akatazwa Kwenda Kwenye Kumbi Za Starehe
Msanii wa Bongo movie na mtangazaji Kajala Masanja ‘Kay’ ameweka wazi kuwa hivi sasa haonekana katika kumbi za starehe usiku wa manane kwa sababu yupo kwenye himaya ya mtu.
Kwa Miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Kajala yupo mbioni kufunga ndoa na mtu mmoja mwenye wadhfa wake ambaye anamuelewa kweli Kajala.
Kwenye mahojiano na gazeti la Amani hivi karibuni, Kajala alisema watu wengi wamekuwa wakimuuliza kwa nini haonekani kwenye kumbi mbalimbali za starehe lakini kikubwa ni kwamba anamheshimu sana mtu aliyenaye kwenye uhusiano kwa sasa na ndiyo maana ameamua kujituliza.
Unajua kuna kipindi mambo yanabadilika kabisa na unafanya vitu vingi kulingana na wakati uliokuwepo, mimi sasa hivi nipo na mtu ambaye hapendi kabisa vitu hivyo vya kutokatoka usiku lakini pia hata mimi mwenyewe nimebadilisha maisha yangu siyo yale tena”.
Kajala alikataa na kudai hamna ndoa inayofungwa hivi karibuni lakini alikiri yupo na mwanaume anayempenda na amedai huvi karibuni atamuweka wazi na kila mtu atamjua.