Shamsa Ford Adai Hajali Kuchukiwa na Watu Ilimradi Anapendwa na Mumewe
Msanii wa filamu za kibongo Shamsa Ford amefunguka na kusema hajali kama watu watamchukia kwa muonekano wake au hata kusema ukweli inapobidi ilimradi anapendwa na mume wake Chidi Mapenzi inatosha.
Shamsa amekuwa Kwenye headlines za mitandao ya kijamii tangu avae gauni lililokuwa fupi sana Kwenye arobaini ya mtoto wa Zamaradi Mketema wiki iliyopita.
Kwenye mahojiano na gazeti Amani baada ya watu wengi kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutokelezea na nguo fupi kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, na kusema kuwa ni ngumu kumridhisha kila mtu kwenye maamuzi yako.
Mimi Mungu kanijalia maneno sijali kabisa na isitoshe Chidi akinipenda na akakubaliana na maamuzi yangu kwangu inatosha kabisa siwezi kumridhisha kila mtu”.