Master J Adai Ma-Prodyuza Hawalipwi Vizuri Kama Zamani
Producer mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Joseph Kimario maarufu kama Master J amefunguka na kuweka wazi kuwa watayarishaji wa muziki wa sasa hawalipwi vizuri kama ilivyokuwa kwao siku za nyuma.
Master J alijizolea umaarufu kutokana na kutengeneza hits songs kibao kwa wasanii wakongwe Kupitia Music Label yake ya MJ Records.
Kwenye mahojiano yake na EFM, Master J amefunguka na kusema kwamba kuna watayarishaji wengi wahalipwi vizuri kuliko wale ambao wanalipwa vizuri kidogo.
Maproducer wengi hawapati kitu, yaani msanii akikuheshimu sana atakupa laki mbili au laki tatu lakini hawa wengine wote ni laki kushuka chini wimbo mzima mpaka beat”.
Lakini pia Master J amewataka Maprodyuza kuhakikisha wanakuwa wabunifu ili kutengeneza Muziki utakaosanifu uhalisia wa Bongo fleva:
Kiukweli Muziki wetu umepoteza uhalisia tunakopy sana kutoka kule Nigeria, Maproducer waongeze ubunifu kidogo ili tuweze kuwa na aina ya Muziki wetu . Kwa maana hili sio zuri maana tuna makabila Zaidi ya 120 tunaweza kuchanganya na kupata uhasilia wetu” .
Master J alitangaza kuachana na kutengeneza muziki na kuamua kuangalia biashara zake nyingine na kuwakabidhi MJ Records vijana wengine.