Sister P-Zamani Muziki Ulikuwa Kazi Sahivi Umekuwa Biashara Tu
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva aliyekuwa anafanya miondoko ya kuchana mwanadada Sister P ameibuka na kudai kuwa sahivi muziki umekuwa biashara na sio kazi kama zamani.
Sister P ameiongelea gemu ya Bongo fleva ilivyobadilika na kutofautiana na zamani ambayo walikuwa wanafanya wao ambapo amedai sasahivi vijana hawaimbi bali wanafanya bishara.
Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Media Sister P ameendelea kufunguka yafuatayo:
Utofauti upo mkubwa tu kipindi kile sisi tulikuwa tunafanya kazi enzi zile lakini sahivi naona watoto wanafanya biashara Muziki sahivi umekuwa biashara tofauti na kazi, sisi tulikuwa tunfanya kazi tunaingiza kipato sawa lakini sasa biashara imekuwa kubwa sana hawa watoto wanalipua tu.
Unakuta msanii anafanya kazi leo kesho kaitoa studio zimekuwa nyingi wasanii wamekuwa kibao na wengine wanakuwa kama wanazingua hivi tofauti na kipindi chetu ilikuwa kazi mpaka kutoka lakini sahivi mtu anakutupuka anaenda studio anatia voko kesho anaamka na nyimbo imetoka na watu wanaisikiliza”.
Sister P alijizolea umaarufu miaka ya nyuma Kupitia wimbo wake wa ‘Anakuja’ lakini pia kutokana na bifu lake na msanii mwenzake Mwanadada Zay B.