Mr. Blue Awainulia Mikono Ali Kiba na Diamond
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khery Sameer au maarufu kama Mr. Blue amewainulia mikono mastaa wa Bongo fleva Diamond na Ali Kiba.
Mr. Blue amefunguka na kuweka wazi kuwa anaona kabisa kuna vitu vya Ziada vinavyowafanya Ali Kiba na Diamond wazidi kupata mafanikio katika tasnia hii.
Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mr Blue amesema wanamuziki wengi chipukizi hutamani kuwa kama wawili hao bila kufahamu mbali na kufanya muziki wanajituma, wana nidhamu na wana malengo ya kufika
Unajua wengi hutamani kuwa kama fulani kwenye muziki hasa watu wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa kama Diamond na Kiba, lakini bila kufahamu kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na vitu vya ziada mbali na kuimba kawaida.
Kwa ushauri wangu, wanamuziki chipukizi waangalie ni vitu gani vya ziada wanavyo wanamuziki wanaotamani kuwa kama wao wavifuate na wataweza kufika kule wanako kuhitaji”.
Ni wiki chache tu zilizopita Mr. Blue alikana taarifa za kuwa ana bifu na Diamond baada ya tetesi za muda mrefu zilizodai hivyo.