Irene Uwoya Aapa Kutoifuta Tatoo Ya Masogange
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakuja kuiguta tatoo ya marehemu Masogange aliyekuwa rafiki yake kipenzi.
Agnes Masogange aliaga dunia mwezi uliopita baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa pumu enzi za uhai wake yeye na Uwoya walikuwa marafiki wakubwa sana.
Mara baada ya tu ya Agnes kufariki Irene Uwoya alienda kucheza tatoo Kwenye mkono wake kwa ajili ya kumkumbuka shoga yake huyo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Uwoya amefunguka kuwa aliichora tatoo hiyo kwa kuwa ni jambo lililotoka moyoni mwake na lilitokana na uchungu aliokuwa nao wa kupitiliza kwa rafiki yake huyo hivyo hawezi kuifuta.
Nitaanzaje kuifuta? Ni kitu ambacho nime-kichora mwen-yewe, tena cha kumbukumbu muhi-mu kwenye maisha yangu, jamani itaendelea kudumu kwenye mkono wangu daima“.